Ni sare ya bao 1-1 kati ya Yanga na Biashara United, mchezo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Yanga wametangulia kwa bao la Fiston Mayele dakika ya 75, lakini Collins Opare akaisawazishia Biashara United dakika tatu baadaye (dakika ya 78). Haya hapa magoli pamoja na mtetemo wa aina yake kutoka kwa shabiki jukwaani akiungana na Fiston Mayele.