Yanga imeichakaza Stand United kutoka Championship mabao 8-1, manne yakitoka kwa Stephane Aziz Ki.... ukiwa ni mchezo wa robo fainali Kombe la Shirikisho la CRDB Bank uliopigwa KMC Complex, Dar es Salaam. Magoli mengine yametoka kwa Clatous Chama aliyefunga mawili, Nickson Kibabae goli la pili na Kennedy Musonda goli la nane..... Goli la kufutia machozi kwa Stand United limefungwa na Msenda Senda dakika ya 49.