Content removal request!


HIGHLIGHTS: AS MANIEMA 0-2 GREEN EAGLES (MSHINDI WA TATU CECAFA KAGAME CUP - 21/7/2019)

Timu ya Green Eagles kutoka Zambia imefanikiwa kuchukua nafasi ya tatu kwenye michuano ya Kombe la Kagame inayohitimishwa leo nchini Rwanda. Eagles wamepata nafasi hiyo baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya AS Maniema ya DR Congo katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu uliopigwa kwenye Dimba la Kigali. Magoli ya Eagles yamefungwa na Edward Mwamba dakika ya 28 pamoja na Amity Shamende 69. Timu hizo zimekutana kwenye mchezo huo baada ya AS Maniema kufungwa na Azam FC kwa penati 5-4 huku Eagles wakiwa wamepoteza mchezo wao wa nusu fainali kwa kichapo cha mabao 4-3 kutoka kwa KCCA.