Content removal request!


YA MORRISON YAJIRUDIA YANGA/ GAMONDI ANG’AKA/ SKUDU, ZOUZOUA/ KOCHA ASEC/ MBONA BADO/ MTAONA MENGI

Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Miguel Angel Gamondi amesema kwa sasa Kiungo Mshambuliaji ‘Winga’ wake Mahlatsi Makudubela ‘Skudu’ hayupo kwenye mipango yake na amempa programu maalum kwa ajili ya kumuweka sawa kabla hajaanza kumtumia kwenye kikosi chake huku akisema hakuna mchezaji aliye juu ya timu. Skudu alijiunga na Young Africans kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Mallumo Gallant ya Afrika Kusini, ambapo tangu amejiunga na timu hiyo amefanikiwa kucheza mechi moja ya kimashindano kabla ya kuumia goti ambalo lilimpelekea arejee kwao Afrika Kusini kabla ya kurudi tena nchini juma lililopita. -- Dar24 ni chanzo namba moja cha habari kwa watanzania mahali popote walipo duniani. Kwa habari za uhakika kutoka nyanja mbali mbali. JE, NA WEWE UNA HABARI? ⚫️ WASILIANA NA DAR24 MEDIA: +255 679 979 786 ⚫️ Email: dar24newsroom@gmail.com ⚫️ Website: www.dar24.com ⚫️ Instagram: @Dar24news ⚫️ Facebook: @dar24 ⚫️ Twitter: @Dar24News #yangasc #asecmimosas #gamondi