Tazama jinsi ambavyo Azam FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa katika dimba la Azam Complex Chamazi, kuanzia saa 1;00 usiku. Mchezo ulikuwa mkali, ambapo Mbao FC licha ya kupaki basi kipindi cha kwanza, walikuwa wakifanya mashambulizi ya kushtukiza na kuambulia kosakosa za hapa na pale na hivyo kwenda mapumziko kukiwa hakuna bao. Mabadiliko ya kocha wa Azam FC kumuingiza Idd Kipagwile kuchukua nafasi ya Joseph Mahundi ndiyo yaliyozaa matunda, Idd Kipagwile akifunga bao la kwanza dakika ya 63 na Bernard Arthur akifunga bao dakika ya 72, huku bao pekee la Mbao likifungwa dakika ya 90 na James Msuva.