Content removal request!


MAGOLI YOTE: AZAM FC 3-1 STAND UNITED (TPL - 04/12/2018)

Timu ya Azam FC imepata ushind wa mabao 3-1 dhidi ya Stand United katika mchezo a Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi Dar es Salaam. Magoli yote yamefungwa kipindi cha pili, Stand wakitangulia kupitia kwa Hafidh Musa dakika ya 53, na kisha Azam wakarejea mchezoni na kupata mabao yao kupitia Yahya Zayd aliyefunga mawili, dakika ya 72 kwa penati na dakika ya 85 huku bao la kusawazisha la Azam FC likiwa limefungwa na Enock Atta.