Content removal request!


DAKIKA 90 (26/8/2019): Kisa cha Simba kutolewa mapema Ligi ya Mabingwa Afrika (UCHAMBUZI)

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC wametupwa nje ya michuano ya Mabingwa barani Afrika (CAF CL) baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na UD Songo kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Je, nini kimeiangusha Simba kwenye michuano hiyo ambayo katika msimu uliopita ilifikia hatua ya robo fainali? Kipindi hiki pia kimefanya uchambuzi wa mechi ya Azam vs Fasil Kenema, na Township Rollers vs Yanga, zilizoshuhudia Yanga na Azam zikisonga mbele kwenye michuano hiyo. Kwenye kipindi hiki pia utashuhudia mapokezi ya Yanga kwenye Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam ikitokea nchini Botswana. Wachambuzi ni Thobias Sebastian na Charles Abel chini ya Ahmed Ally. Sehemu ya pili ya kipindi ni dakika 30 za kuitazama Ligi Daraja la Kwanza, leo tukiwa na Mwenyekiti wa Cosmopolitan Said Rajab.