Content removal request!


SINGIDA UNITED 2-2 JKT TANZANIA: HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (TPL - 12/05/2019)

Singida United imetoshana nguvu na JKT Tanzania kwa kufungana mabao 2-2 kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) Wenyeji hao ndiyo waliokuwa wakitangulia kufunga na wageni kufanya kazi ya kuchomoa, magoli yote ya Singida United yakifungwa na Habibu Haji Kyombo dakika ya 30 na 50 huku magoli ya JKT yakifungwa na Dickson Chota dakika ya 45+4 na Samwel Kamuntu dakika ya 78. Matokeo hayo yameifanya JKT Tanzania kufikisha pointi 41 na kukaa nafasi ya 16 huku Singida United wakiwa na pointi 45 katika nafasi ya nane.