Content removal request!


MAGOLI: SIMBA SC 3-0 SINGIDA UNITED; (TPL – 29/12/2018)

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC wameendeleza ubabe kwa Singida United baada ya leo kuishushia kipigo cha mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa usiku wa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo uliokuwa na burudani ya aina yake kwa timu zote kushambuliana kwa zamu, Simba ilianza kujipatia bao la kwanza dakika ya 18 kupitia kwa Nahodha John Bocco aliyemalizia vema pasi ya Shiza Kichuya na kufanya kipindi cha kwanza kimalizike kwa Simba kuwa mbele kwa bao 1-0. Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kuzidisha mashambulizi licha ya Singida kupoteza nafasi kadhaa, na Shiza Kichuya kuibuka shujaa kwa kufunga mabao mawili dakika ya 49 na 55 magoli yote akitumia pasi za Clatous Chama. Ushindi huo unaifanya Simba ijiongezee pointi tatu na kufikisha pointi 33 ikiendelea kusalia katika nafasi yake ya tatu nyuma ya Azam yenye pointi 40 na Yanga yenye pointi 50 kileleni.