Azam FC 0-3 Simba SC | Magoli, Penati, Off-side | NBC Premier League 09/05/2024 by @Azam TV - Post Details

Azam FC 0-3 Simba SC | Magoli, Penati, Off-side | NBC Premier League 09/05/2024

MZIZIMA DERBY: Simba FC imeshinda 3-0 dhidi ya Azam FC, mchezo wa ligi kuu ya NBC ukipigwa kwenye Dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam. Magoli yote yamefungwa kipindi cha pili akianza Sadio Kanoute dakika ya 63, Fabrice Ngoma dakika ya 77 na David Kameta dakika ya 89. Azam FC walipata penati mapema lakini walikosa kupitia kwa Feisal Salum.... lakini pia kuna utata kuhusu tukio la Azam kupata goli iliyoamuliwa kuwa ilikuwa ni off-side.

Similar Posts!

Simba SC 0-0 Mogadishu City Club | Highlights | CECAFA Kagame Cup 24/07/2026
Simba SC 0-0 Mogadishu City Club | Highlights | CECAFA Kagame Cup 24/07/2026

Simba SC imekabwa koo na kulazimishwa suluhu na Mogadishu City Club ya Somalia, katika mchezo wake wa kwanza wa Kombe la Kagame 2026, ukipigwa kwenye Dimba la Kigali, Rwanga. Kwenye mchezo huu Simba imewatumia baadhi ay nyota wake wapya akiwemo Ibrahim Doumbia , Cooper, Kelvin Nashon na wengine. Tazama highlights.



Ally Kamwe azungumzia tetesi za Aziz Ki kurejea Yanga
Ally Kamwe azungumzia tetesi za Aziz Ki kurejea Yanga

KAMWE AKWEPA KUMZUNGUMZIA AZIZ KI: Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe anasema hakuna timu Afrika ambayo haipendi kuwa na mchezaji mwenye daraja la Stephane Aziz Ki, japo amekwepa kuzungumzia kwa undani tetesi zinazomhusisha kurejea mitaa ya Jangwani. Kamwe pia amesema kuna mchezaji walimpandisha thamani makusudi ili watu walipe hela nyingi. Kamwe amesema hayo leo kwenye mahojiano maalumu kupitia kipndi cha U-LIVE cha @ufmradiotz #YangaSC #Kamwe #UFM #ULIVE



Simba SC 1-0 Azam FC | Highlights | Fainali | CRDB Bank Federation Cup 04/07/2026
Simba SC 1-0 Azam FC | Highlights | Fainali | CRDB Bank Federation Cup 04/07/2026

Simba SC imenyakua Kombe la Shirikisho la CRDB Bank kwa kuichapa Azam FC bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliopigwa kwenye Dimba la Gombani Pemba. Goli pekee la ubingwa limefungwa Yahya Zayd ambaye amejifunga dakika ya 62.



JKT Tanzania 0-3 Yanga SC | Highlights | NBC Premier League 30/06/2026
JKT Tanzania 0-3 Yanga SC | Highlights | NBC Premier League 30/06/2026

Yanga SC imehitimisha msimu wa Ligi Kuuya NBC 2025/26 kwa kishindo, ikiichapa JKT Tanzania mabao 3-0 kwenye Dimba la Meja Jenerali Isamuhyo na kutwaa ubingwa wa tano mfululizo. Magoli yamefungwa na Prince Dube, Maxi Nzengeli na Laurindo Dilson Maria Depu.



Hat-trick ya Okello | Yanga SC 3-0 TRA United | NBC Premier League 27/06/2026
Hat-trick ya Okello | Yanga SC 3-0 TRA United | NBC Premier League 27/06/2026

Allan Okello 'Star Boy', amepiga magoli yote matatu #Hattrick , Yanga ikishinda 3-0 dhidi ya TRA United, mchezo wa raundi ya 29, Ligi Kuu ya NBC, uliopigwa KMC Complex, Dar es Salaam. Haya hapa magoli yote.



Yanga 3-0 Azam FC | Highlights | NBC Premier League 24/06/2026
Yanga 3-0 Azam FC | Highlights | NBC Premier League 24/06/2026

Yanga SC imezidi kuusogelea ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu, kwa kuwachapa Azam FC mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar. Magoli ya Yanga yamefungwa na Ibrahim Abdullah 'Bacca', Laurindo Dilson Depu, na Pacome Zouzoua. Hii ni Ligi Kuu ya NBC, raundi ya 28 (bado mbili tu) Tazama highlights



Magoli | Yanga SC 3-0 Azam FC | NBC Premier League 24/06/2026
Magoli | Yanga SC 3-0 Azam FC | NBC Premier League 24/06/2026

Yanga SC imezidi kuusogelea ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu, kwa kuwachapa Azam FC mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar. Magoli ya Yanga yamefungwa na Ibrahim Abdullah 'Bacca', Laurindo Dilson Depu, na Pacome Zouzoua. Haya hapa magoli yote...