Kati ya Ronaldo na Messi nani mkali? by @BBC News Swahili - Post Details

Kati ya Ronaldo na Messi nani mkali?

Lionel Messi ameendelea kuandika historia kwa herufi kubwa baada ya kuiongoza Argentina kupata ushindi muhimu dhidi ya Austria. Licha ya kukosa penalti mapema, nahodha huyo alionyesha utulivu na ubora wake kwa kufunga mabao mawili yaliyohakikisha timu yake inaondoka na pointi zote. Uchezaji wake umeendelea kuthibitisha kwa nini wengi humchukulia kuwa miongoni mwa wachezaji bora kuwahi kutokea duniani. Mafanikio hayo yameongeza uzito kwenye mjadala wa muda mrefu kati yake na Cristiano Ronaldo. Wakati Ronaldo akisifiwa kwa uwezo wake wa kufunga na kudumu kileleni kwa miaka mingi, Messi anaendelea kuvunja rekodi na kuacha alama kubwa zaidi katika michuano mikubwa. Je, ushindi huu na rekodi anazoendelea kuweka zinatosha kumfanya awe juu ya mpinzani wake wa muda mrefu? Mwandishi wa BBC @kenanivictorna taarifa zaidi 🎥: @frankmavura #bbcswahili #fypシ゚viral #tanzaniantiktok🇹🇿 #kenyantiktok🇰🇪 #kombeladunia2026 Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw

Similar Posts!

Vozinha: Kipa "mzee" aliyeiteka dunia ya soka.
Vozinha: Kipa "mzee" aliyeiteka dunia ya soka.

Alikuwa shujaa wa Cape Verde. Alionesha kiwango cha hali ya juu na kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi katika sare ya 0-0 dhidi ya Hispania kwenye Kombe la Dunia la FIFA. Mafanikio hayo yalikuwa na maana kubwa zaidi kwa Vozinha kuliko ambavyo wengi wangeweza kufikiria. #bbcswahili #kombeladunia #fifa Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw



Kwanini Afrika iliishangilia Mexico dhidi ya Afrika Kusini?
Kwanini Afrika iliishangilia Mexico dhidi ya Afrika Kusini?

Kwanini Afrika iliishangilia Mexico dhidi ya Afrika Kusini katika mechi ya Kombe la Dunia? Baadhi ya mashabiki barani Afrika waliamua kuishangilia Mexico dhidi ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) katika mechi ya ufunguzi ya Kombe la Dunia 2026 kama njia ya kupinga chuki na mashambulizi ya kibaguzi dhidi ya wageni. Je, michezo inapaswa kutenganishwa na siasa na migogoro ya kijamii au haya ndiyo matokeo ya kile kinachoendelea Kusini? #bbcswahili #mexico #afrikakusini Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw



Kim Jong Un akutana na  timu ya wanawake Korea Kaskazini
Kim Jong Un akutana na timu ya wanawake Korea Kaskazini

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amekutana na kuwapongeza wachezaji wa klabu ya wanawake ya Naegohyang waliotwaa ubingwa wa Asia, pamoja na timu ya wasichana chini ya miaka 17, ambapo wote walionyesha furaha kubwa na hata kulia kwa hisia. Timu hiyo pia ilishinda dhidi ya timu ya Japan na imefuzu mashindano ya kimataifa yajayo, jambo linaloonyesha mafanikio makubwa ya soka la wanawake nchini Korea Kaskazini. #bbcswahili #kimjongun🇰🇵 #koreakaskazini Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw



Mafahali wa Kariakoo
Mafahali wa Kariakoo

Joto linazidi kupanda nchini Tanzania kuhusu pambano maarufu la soka la watani wa jadi, Yanga na Simba lililopangwa kufanyika Juni 15 jijini Dar es Salaam. - Mamlaka za soka zinasisitiza pambano kufanyika huku Yanga ikisema haichezi, ikipinga inachokiita mchezo wa awali wa Machi 8 kuaihirishwa kiholela. - Sasa tuangalie badhi ya maamuzi magumu yaliyowahi kufikiwa kuhusu Yanga ama Simba ndani ya miaka 20 - - - 📸@simbascofficial 📸@Young Africans Sports Club #bbcswahili #michezo #soka#simba#mpira #yanga Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw