Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC wamepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ilopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Wenyeji Mbeya City ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 22 kupitia kwa Iddy Selemani ‘Naldo’ kabla ya Simba kufanya mabadiliko na kurejea mchezoni kipindi cha pili wakipata mabao mawili kupitia kwa Jonas Mkude dakika ya 68 na Meddie Kagere dakika ya 85. Matokeo hayo yameifanya Simba ifikishe pointi 75 katika michezo 29 iliyocheza ikiwa na pointi tano nyuma ya wapinzani wao wa jadi Yanga SC wenye pointi 80 katika mechi 34 huku Azam wakiendelea kubaki nafasi ya tatu na pointi zao 66.
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, Yanga SC wamepoteza mchezo kwa mara ya kwanza msimu huu, wakichapwa 3-2 na Dodoma Jiji, mchezo, mchezo ukipigwa Airtel Stadium, Singida. Magoli ya Yanga yamefungwa na Allan Okello dakika ya 2 na 41, huku magoli ya Dodoma Jiji yakitoka kwa Bakari Mwamnyeto aliyejifunga dakika ya 29, Mwana Kibuta David dakika ya 90 na Wazir Junior Shemtembo dakika za nyongeza. Haya hapa magoli yote..
#NBCPL: Tazama magoli yote matano yaliyofungwa kwenye mchezo wa NBC Premier League kati TRA United dhidi ya Azam FC. FT: TRA United 4-1 Azam FC Magoli ya TRA United yamefungwa na Ally Ng'azi, Ammy Mapaka na Ramadhan Salum 'Chobwedo' Goli la Azam FC limefungwa na Jephte Kitambala Bola. #NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #ImenogaZaidi #TRAUnitedvsAzamFC #TRAUnited #AzamFC #TRAUnitedAzamFC
KARIAKOO DERBY | Imepigwa dabi moja ya maana sana kwenye Dimba la Amaan, Zanzibar, Yanga na Simba wakimaliza dakika 90 bila bao, lakini burudani za kutosha. Hii ni mechi ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania
Yanga SC imeichakaza JKT Tanzania mabao 5-0 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa leo kwenye Dimba la KMC Complex, Dar es Salaam. Wafungaji wa magoli haya ni Mohamed Hussein Zimbwe Jr,, Aurellio Depu, Mudathir Yahya, Prince Dube na Shekhan Ibrahim.
Ni mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA iliyopigwa kwenye Dimba la Al Salaam, Cairo nchini Misri, na timu ya taifa ya Tanzania #TaifaStars kuchwa 4-3 na Kuwait. Magoli ya Tanzania yamefungwa na M’mombwa 6’, 87’, na Taryin Allarakhia 34’ huku ya Kuwait yakitoka kwa Daham 46’, 52’ Nasser 63’ na Hamdan 69’
KMC vs SINGIDA BS: Kocha Marcio Maximo wa KMC, amesema mataifa ya Argentina na Brazil ni wapinzani ndani ya uwanja, ...
KARIAKOO DEEBY | Fahamu ukweli kuhusu matukio yote yaliyozua utata kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Simba uliopigwa Septemba 16, 2025. Moja kati ya matukio yaliyozua gumzo ni goli pekee walilofunga Yanga na kuamua mshindi wa Ngao ya Jamii 2025. Osman Kazi na jopo lake wanamaliza utata kwa kutumia sheria na kanuni za soka
KUTOKA CAIRO MISRI: " ....msimu huu tunahitaji kuwapiku Yanga" Baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Wadi Degla FC inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo, Kocha wa Simba, Fadlu davids anaeleza baadhi ya mambo ambayo ameridhika nayo, na maeneo ambayo bado ana kazi ya kufanya.... Kuhusu kikosi chake, Kocha Fadlu anasema bado wanahitaji angalau mchezaji mmoja mwenye kitu cha ziada (X-Factor) atakayewaongezea kitu hasa kwenye michuano ya kimataifa pamoja na mbio za ubingwa wa #NBCPremierLeague msimu ujao wakilenga kuwa juu ya Yanga ... Fadlu anasema anaamini mdhamini wao upande wa jezi, 'Jayruty', atalimaliza hilo.... Naye mfungaji wa moja kati ya magoli mawili ya Simba, Kibu Denis anazungumza machache kuhusu maendeleo ya kambi nchini Misri.... Patrick Nyembera anakuja na taarifa kamli kuhusu mchezo huo... #SimbaSC #SimbaEgypt #SimbaPreSeason