Extra Online Tv's user profile page. Match highlights, posts and more on site!

“”

 Report User

Highlights

SIMBA YAIKIMBIZA YANGA NDANI YA DK 450, KAZI JULAI 3|Simba kuimaliza Yanga?
SIMBA YAIKIMBIZA YANGA NDANI YA DK 450, KAZI JULAI 3|Simba kuimaliza Yanga?

ZIKIWA zimebeki siku tatu kwa watani wa jadi, Simba na Yanga kukutana Uwanja wa Mkapa, rekodi zinaonyesha kuwa makocha wawili Didier Gomes wa Simba na Nassredine Nabi wa Yanga walikuwa na kazi ya kukimbizana ndani ya dk 450. Kwenye mechi zao tano za hivi karibuni kwenye ligi Gomes alionekana kumkimbiza Nabi kwa kusepa na pointi nyingi ambazo ni 15 huku Nabi akisepa na pointi zake 10. Ni Gomes raia wa Ufaransa alishinda mechi zake 5 alizokaa kwenye benchi na alishuhudia jumla ya mabao 14 wachezaji wake wakifunga na mabao matatu waliokota kwenye nyavu zao. Ndani ya dakika 450 msako wa pointi 15 Simba ilisepa na pointi zote mazima ambapo ugenini ilikuwa kwenye mechi tatu na nyumbani ilikuwa kwenye mechi mbili. Mwendo wa Gomes ulikuwa namna hii:-Aprili 27, Simba 3-1 Dodoma Jiji,Uwanja wa Mkapa, Mei 29, Namungo 1-3 Simba,Uwanja wa Majaliwa, Juni 3, Ruvu Shooting 0-3 Simba, uwanja wa CCM Kirumba, Juni 19, Polisi Tanzania 0-1 Simba, Uwanja wa CCM Kirumba, Juni 22, Simba 4-1 Mbeya City, Uwanja wa Mkapa. Kwa upande wa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi katika mechi tano ambazo ni dk 450, Yanga ilipoteza mchezo mmoja, sare moja na ushindi katika mechi tatu. Ilikuwa msako wa pointi 15, Nabi alisepa na pointi 10 na kuyeyusha pointi tano mazima huku wachezaji wake wakifunga jumla ya mabao 8 na kufungwa mabao matano. Mwendo wake ulikuwa namna hii:-Aprili 25, Yanga 0-1 Azam FC, Uwanja wa Mkapa, Mei 15, Namungo 0-0 Yanga, Uwanja wa Majaliwa, Mei 19, JKT Tanzania 0-2 Yanga, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, Juni 17, Ruvu Shooting 2-3 Yanga, Uwanja wa Mkapa, Juni 20, Yanga 3-2 Mwadui FC.



KOCHA WA SIMBA ATANGAZA MFUMO ATAKO WAMALIZA NAO YANGA JULY 3 MKAPA
KOCHA WA SIMBA ATANGAZA MFUMO ATAKO WAMALIZA NAO YANGA JULY 3 MKAPA

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes amefunguka kuwa siri kubwa ya ubora kikosi chake katika kuchezea mpira inatokana na balansi inayoletwa na matumizi ya viungo wawili wakabaji, kulinganisha na wanapotumia kiungo mmoja pekee. Ndani ya kikosi cha Simba, Gomes amekuwa akiwatumia zaidi Taddeo Lwanga na Mzamiru Yassin kama pacha ya viungo wakabaji ndani ya kikosi chake katika michezo mingi, hali inayowapa urahisi viungo wa juu wa Simba kuwa na wakati mzuri wa kuchezea mpira.   Akizungumza na Extra online tv Gomes alisema: “Tumekuwa tukitumia mifumo mbalimbali kuendana na wapinzani ambao tunakutana nao, lakini naweza kusema kikosi chetu kinakuwa na balansi kubwa na kucheza vizuri zaidi iwapo tunacheza na viungo wawili wakabaji. “Lakini kuna wakati tunalazimika kujitoa mhanga kwa kutumia kiungo mmoja pekee hasa tunapotumia mfumo wa 3-5-2, kama ambavyo tulicheza dhidi ya Mbeya City," . Mchezo ujao wa Simba ni dhidi ya Yanga unatarajiwa kuchezwa Julai 3, Uwanja wa Mkapa saa 11:00 jioni.



HIVI NDIVYO KOCHA GOMES WA SIMBA SC ANAVYOFIKIRIA KUHUSU YANGA"VPL NA FA TUNABEBA"
HIVI NDIVYO KOCHA GOMES WA SIMBA SC ANAVYOFIKIRIA KUHUSU YANGA"VPL NA FA TUNABEBA"

HASIRA za Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes kwa sasa zipo katika kubeba makombe mawili ya ndani ambayo anashindania sambamba na watani zao wa jadi, Yanga.   Gomes amepania kumaliza msimu huu kwa kutetea mataji yao waliyoyatwaa msimu uliopita ambayo ni Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam.   Tayari ndani ya Ligi Kuu Bara, Simba ndiyo vinara wakiwa na pointi 61 baada ya kucheza mechi 25. Mbio zao za kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika zilikwama Mei 22 baada ya kutolewa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 4-3 ambayo Simba ilifunga.    Gomes amesema: “Kikubwa ni kuangalia namna ya kutetea mataji yetu msimu huu, haitakuwa rahisi kwetu kuona tunayapoteza na kwenda sehemu nyingine.   "Tutapambana kwa nguvu zote kutetea mataji yetu kwani malengo yetu ni kuona kwamba tunabeba mataji yote ambayo tutashiriki kwa sasa,". Msimu huu ikitokea Simba ikabeba tena mataji hayo, itakuwa ni msimu wa nne mfululizo Yanga inakosa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam. #KochaGomez #SimbaSc




« Previous


User Detail Page

You can find user latest posts and related content on the page. Friends, comments for events / matches are also available on the page. Even you can find users who are same pleasure with current user.

#Travel, #SupportYourTeam, #AllAboutSports