KOCHA WA SIMBA ATANGAZA MFUMO ATAKO WAMALIZA NAO YANGA JULY 3 MKAPA by @Extra Online Tv - Post Details

KOCHA WA SIMBA ATANGAZA MFUMO ATAKO WAMALIZA NAO YANGA JULY 3 MKAPA

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes amefunguka kuwa siri kubwa ya ubora kikosi chake katika kuchezea mpira inatokana na balansi inayoletwa na matumizi ya viungo wawili wakabaji, kulinganisha na wanapotumia kiungo mmoja pekee. Ndani ya kikosi cha Simba, Gomes amekuwa akiwatumia zaidi Taddeo Lwanga na Mzamiru Yassin kama pacha ya viungo wakabaji ndani ya kikosi chake katika michezo mingi, hali inayowapa urahisi viungo wa juu wa Simba kuwa na wakati mzuri wa kuchezea mpira.   Akizungumza na Extra online tv Gomes alisema: “Tumekuwa tukitumia mifumo mbalimbali kuendana na wapinzani ambao tunakutana nao, lakini naweza kusema kikosi chetu kinakuwa na balansi kubwa na kucheza vizuri zaidi iwapo tunacheza na viungo wawili wakabaji. “Lakini kuna wakati tunalazimika kujitoa mhanga kwa kutumia kiungo mmoja pekee hasa tunapotumia mfumo wa 3-5-2, kama ambavyo tulicheza dhidi ya Mbeya City," . Mchezo ujao wa Simba ni dhidi ya Yanga unatarajiwa kuchezwa Julai 3, Uwanja wa Mkapa saa 11:00 jioni.

Similar Posts!

SimbaSC  ikimchaKAZA Asec Mimosa 3-1,Tazama magoli yote,Sakho,Banda,Kapombe,Simba vs Asec, Simba leo
SimbaSC ikimchaKAZA Asec Mimosa 3-1,Tazama magoli yote,Sakho,Banda,Kapombe,Simba vs Asec, Simba leo

Sakho Nascimento Pele. Goli la Pele lilifungua kinywa pale kwa mkapa liliashiria leo itakuwa siku njema na kesho Valentine itakuwa ni kumwaga na kuchota upendo kwasababu hakika jua linazama likiwa na tabasamu maridhawa,likiwa linaushahidi kwamba rangi Nyekundu ni ya kipekee. Pia goli hili la Pele limeacha uchungu,limeacha huzuni kwasababu Kuna upande ulikuwa unaomba Mwana wa Kondoo kunyongwa,Mwana wa Kondoo kupewa chakula kibaya na zaidi kufukuzwa zizini. Wakati Jua linaenda kuzama dunia nzima inafahamu kuna Pele mmoja yule wa Brazil yule ambaye ni mfalme wa soka lakini pale Kijiji kwetu msimbazi tunamjua Pele mmoja ambaye Mara nyingi tunamuita kwa heshima yote yaani Sakho Nascimento Pele kwasababu goli lake la bicycle kick limeleta furaha kwa yule shabiki aliyevaa jezi nyekundu,limeleta huzuni kwa yule shabiki aliyevaa jezi ya Njano.