Bongo5's user profile page. Match highlights, posts and more on site!“” Report User |
Rekodi ya Simba SC dhidi ya Azam FC ni ya kuvutia baada ya kukutana mara 29, katika mashindano yote Ligi Kuu , Kombe la Mapinduzi, Azam Sports Federation Cup, Kombe la Kagame, Kombe la Ujirani Mwema, Kombe la Banc ABC Super 8 na Ngao ya Jamii. Simba SC imeshinda mara 13 ikiwa ni pamoja na leo, Azam FC ikishinda 10 na mechi 6 zikimalizika kwa sare.
Ligi Kuu soka Tanzania Bara imeendelea hii leo katika Uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera, klabu ya Simba imechomoza na ushindi wa mabao 2 – 0 dhidi ya Kagera Sugar.
Nahodha wa timu ya Singida United inayodhaminiwa na kampuni ya michezo ya kubashiri SportPesa, Mudathir Yahya amedai wameshinda mchezo wao dhidi ya Mbao FC baaba ya kufanya marekebisho ya mchezo wao uliopita ambao walifungwa. Katika mchezo huo uliochezeka katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma, Singida iliondoka na ushindi wa goli mbili kwa moja dhidi ya Mboa Fc.