Ford TV Tanzania's user profile page. Match highlights, posts and more on site!“” Report User |
Baada ya kufanikiwa kuitoa Township Rollers kwenye hatua ya awali Klabu Bingwa Afrika, Yanga SC sasa katika raundi ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika watacheza dhidi ya Zesco United ya Zambia. Ikumbukwe Zesco United wamefika hatua hiyo baada ya ushindi wa jumla ya goli 3-0 dhidi ya Green Mamba ya Eswatini. Yanga SC wataanzia nyumbani Tanzania na kumalizia ugenini nchini Zambia, mechi ya kwanza itapigwa kati ya Septemba 13-15 marudiano kuchezwa kati ya Septemba 27-29 mwaka huu. Baada ya hapo, mshindi wa hatua hii atafuzu katika hatua ya makundi ya michuano hiyo ya Afrika.
ZIKIWA zimebaki takribani siku nne kabla ya Simba kuivaa UD do Songo kutoka Msumbuji, rekodi zinaonyesha kuwa Simba wana asilimia kubwa ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, Jumapili ya wiki hii. Tangu msimu uliopita, Simba katika michuano ya kimataifa haijapoteza mchezo wowote waliocheza kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ambao ndiyo uwanja wanaoutumia kwa mechi zao za nyumban Katika mchezo huo wa marudiano, Simba inaingia ikiwa na rekodi ya kushinda michezo mitano ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita kati ya sita iliyocheza hapo ambapo mmoja pekee ilitoka suluhu. Michezo ambayo Simba ilibuka na ushindi walipocheza nyumbani kwenyeUwanja wa Taifa ni; Simba 4-1 Mbabane Swallows, Simba 3-1 Nkana, Simba 3-0 JS Saoura, Simba 1-0 Al Ahly na Simba 2-1 AS Vita Club. Ule wa suluhu ni dhidi ya TP Mazembe. Simba na UD Songo zilipokutana Msumbiji, matokeo yalikuwa suluhu jambo ambalo linaipa nafasi kubwa Simba kusaka ushindi ili isonge hatua inayofuata.