Content removal request!


Magoli AZAM 2 - 0 GOR MAHIA Kagame Cup

AZAM FC imefanikiwa kwenda Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Azam FC sasa watasubiri mshindi kati ya Simba SC na JKU ya Zanzibar ikutane naye fainali Ijumaa hapa Taifa kujaribu kutetea taji lake ililolitwaa mwaka 2015 Dar eds Salaam pia. Lakini haukuwa ushindi mwepesi, kwani Azam FC ililazimika kusubiri hadi dakika 30 za nyongeza kupata tiketi ya kwenda fainali, baada ya kubanwa kwa sare ya 0-0 ndani ya dakika 90. Mabao ya Azam FC ambayo leo ilimkosa kinara wake wa mabao, Shaaban Iddi Chilunda yamefungwa na Ditram Nchimbi dakika ya 92 na beki Mzimbabwe, Bruce Kangwa dakika ya 100.