Content removal request!


VIDEO : TAZAMA KOSAKOSA ZA MAGOLI SIMBA VS AL AHLY,GOLI LA AL AHLY LIMESABABISHWA HIVI

Mechi tamu ambayo timu zimeonyesha ubora mpaka filimbi ya mwisho, huwezi kujutia kwanini ulichelewa kulala kama umeshuhudia mechi hii katika dakika zote. Ilikuwa iko wazi kabisa kuwa ni mechi ambayo Ahly alihitaji alama 3 ili kufuta uteja baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo mbele ya Simba. Kuna kitu Gomes amekipandikiza katika fikra za wachezaji wa Simba nako ni kujua kuwa jukumu la kuzuia si la watu fulani wachache ndani ya timu. Wakati ambao Simba haina mpira unaona wachezaji wote wanafanya mikimbio ya haraka kuhakikisha kuwa wanakuwa nyuma ya Mpira. Hiki si kitu ambacho tulikuwa tukikiona huko nyuma, kwanza timu haikuwa na nidhamu hasa wanapoupoteza mpira. Wachezaji wanajigawa mafungu mawili, kuna wale ambao wanazuia na wengine wanaamini kukaba si sehemu ya majukumu yao. Leo Simba ilicheza kwa tahadhari kubwa hasa wakati ambao Ahly wanamiliki mpira, kwanza hawakukubali kuvunja umbo lao na walikubali kuwa wadogo mbele ya mpinzani. Mbele alibaki Meddie Kagere ili kusubiri mashambulizi ya haraka pale ambapo Simba itafanikiwa kuunasa Mpira. Kwa bahati mbaya tu ni kuwa mashambulizi mengi ya Simba yalizuia na Ahly baada ya kuwa compact sana katika eneo lao. Ahly ilishajua kuwa Simba ina wachezaji wawili ambao ni hatari hasa katika eneo la mbele. Kongole kwa Pitso kwa sababu mabadiliko makubwa ya kikosi aliyoyafanya yaliendana na mahitaji ya mchezo wa leo. Ahly ilifanikiwa kuua movement nyingi za Simba kwa kuzuia wachezaji wanaohusika na build up nyingi za Simba. Kwanza ni Luis, wakahakikisha kuwa hawi na madhara kwa kumnyima uhuru wa kufanya mikimbio kutokea pembeni . Wa pili ni Chama, kila aliposhika Mpira kuna wachezaji wawili walimzonga ili kuhakikisha haoni ni wapi aipeleke pasi yake ya kwanza . Kikubwa zaidi wachezaji wa Simba wanajiamini sana wakiwa na mpira, timu nyingi za Tanzania zinapokuwa ugenini huoni wakipiga pasi na kufika katika eneo la mpinzani. Heko kwa Simba, kuna muda waliiweka Ahly katika nyakati ngumu na kama wangeongeza umakini pengine wangeondoka na sare kama sio kushinda mechi kabisa. Ni nafasi moja pekee ambayo imeamua matokeo, mbali na goli hakika Ahly walipewa mechi nzuri na waliulizwa maswali magumu pia.