Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wachezaji wake wamepambana kusaka pointi tatu muhimu mbele ya Dodoma Jiji, jambo ambalo wanahitaji pongezi. Ikiwa Uwanja wa Jamhuri Simba imeshinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji kwenye mchezo wa Kiporo na kusepa na pointi tatu. Bao la kwanza kwa Simba lilipachikwa na Meddie Kagere dakika ya 30 likawekwa usawa na Cleophance Mkandala dakika ya 36 ambaye alionyeshwa kadi ya njano kwa kushangilia akiwa ametoa jezi. Bernard Morrison ambaye aliweza kuanza kwenye mchezo wa kwanza wa Gomes ndani ya Simba katika Ligi Kuu Bara alipachika bao ushindi dakika ya 66 kwa pasi ya Perfect Chikwende. Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 38 ikiwa imeachwa kwa pointi 6 na watani zao wa jadi Yanga wenye pointi 44 wakiwa nafasi ya kwanza. Gomes amesema:"Wachezaji wamepambana kutafuta pointi tatu wanahitaji pongezi hesabu zetu ni mchezo wetu ujao wa Ligi Kuu Bara, " HABARI MPYA DAILY:https://bit.ly/3c3bEDc HABARI ZA MICHEZO: https://bit.ly/2TAgnWx HABARIZA WASANII: https://bit.ly/2X2f84R HABARI ZA SIASA: https://bit.ly/36r0xCW Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/Kidanistars Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars