Content removal request!


Yanga vs Simba, Mwamuzi Saanya Kuchezesha Taifa

Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars Mwamuzi kiboko wa Yanga, Martin Saanya amekabidhiwa kuchezesha mechi ya watani wa jadi Yanga na Simba Jumapili Machi 8, ijayo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga wamekuwa na bahati mbaya na mwamuzi Saanya tangu alipoanza kuchezesha Ligi Kuu Tanzania Bara mara kadhaa wamekuwa wakikwaruzana kutonaka na matukio ya uwanjani. Mwamuzi Saanya mwaka 2009 alikuwa wa akiba wakati Yanga ilipotoka sare na Simba, lakini mwaka 2013 Simba ilipolala mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa ndiye aliyechezesha. Hata hivyo, Saanya aliingia kwenye mzozo na Yanga baada ya kutoa penalti kwa Coastal Union kwenye dakika za lala salama na mechi kumalizika kwa sare ya bao 1-1 kwenye msimu wa 2012/13, jambo ambalo liliifanya Yanga kumchukia na kukosa imani naye. Saanya alifungiwa na Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) mwaka mzima kwa kushindwa kumudu mechi hiyo ambayo ilisababisha mashabiki wa Yanga kuharibu mali za Uwanja wa Mkwakwani pamoja na basi la Coastal Union. Kabla ya mchezo huo, mwamuzi huyo alikuwa akituhumiwa na mashabiki wa Yanga kwamba aliibeba Simba kwenye mechi ya hisani dhidi ya Azam. Simba ilishinda mabao 3-2 huku Azam wakidai kunyimwa penalti mbili za wazi. Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/Kidanistars Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars