Content removal request!


TANZANIA YACHAPWA 1-0 NA LESOTHO NA KUPUNGUZA MATUMAINI YA KUFUZU AFCON

Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars MATUMAINI ya Tanzania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) mwakani yameanza kufifia tena baada ya kuchapwa bao 1-0 na wenyeji, Lesotho jioni ya leo Uwanja wa Setsoto mjini Maseru. Bao lililoizamisha Taifa Stars leo limefungwa na beki wa klabu ya Matlama Maseru, Nkau Lerotholi dakika ya 76 kwa kichwa akimalizia mpira wa kona kutoka upande wa kulia. Kwa matokeo hayo, sasa timu yoyote kati ya tatu, Lesotho, Tanzania na Cape Verde zinaweza kuungana na vinara wa kundi hilo, Uganda kwenda Cameroon katikati ya mwaka ujao. Mamba wa Lesotho wanapanda nafasi ya pili baada ya kufikisha pointi tano sawa na Tanzania, wakati Cape Verde inashika mkia kwa pointi zake nne. Kikosi cha Lesotho kilikuwa; Samuel Khetsekile, Mafa Moremoholo, Basia Makepe, Bokang Sello, Tsoarelo Bereng/Hlompho Kalake dk71, Tsepo Toloane, Thapelo Tale/Sera Motebang dk51, Sepiriti Malefane, Jane Thaba-Ntso/Jane Tsotleko dk70, Tumelo Khutlang na Nkau Lerotholi. Tanzania; Aishi Manula, Abdallah Kheri/John Bocco dk83, Ally Sonso, Aggrey Morris, Kelvin Yondan, Erasto Nyoni, Mudathir Yahya/Feisal Salum ‘Fei Toto’dk73, Himid Mao, Simon Msuva, Shaaban Iddi Chilunda na Gardiel Michael/Shiza Kichuya dk59. Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars