Content removal request!


Mzee Mpili Awachimba Mkwara Simba "Hawatoki Kigoma"

Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars IMBA wanalia wakiwaambia wababe wao Yanga kwamba mumshukuru Mzee wenu Mpili vinginevyo mngekula nyingi lakini mwenyewe amejibu mapigo akiwaambia ‘Hapo mmepigwa na nyuklia moja tu mmesambaratika sasa subirini Kigoma mi natangulia’. Yanga ilicheza kwa mbinu bora zaidi dhidi ya Simba juzi na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 la mapema dakika ya 11 tu kutoka kwa kiungo Zawadi Mauya na kuwacheleweshea Wekundu hao sherehe za ubingwa wa nne mfululizo. Akizungumza jana na Mwanaspoti, Mzee Mpili ambaye ni shabiki wa Yanga kutoka Ikwiriri, Pwani alisema watani wao wana bahati kwani walikuwa wapigwe nyingi katika mchezo wa juzi. Mzee Mpili ambaye alionekana kuwa mwenye furaha akiwa amevaa fulana yake safi akaenda mbali akisema safari ya kuipiga Simba ndio imeanza na sasa anatangulia mkoani Kigoma kuanza maandalizi ya mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) utakaochezwa Julai 25 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika. “Simba wana bahati sana jana (juzi) walikuwa wapigwe nyingi ila tukasema lile linatosha hawana timu ya kutufunga, sisi Yanga kama tuko sawa na tumeshikamana kama ambavyo hali ilivyo sasa ndani ya Yanga. “Hii ni mwanzo tu mimi hapa nimemaliza sasa natangulia Kigoma watanikuta huko wakutane na kipigo kingine wakimaliza mechi zao watanikuta kule nawasubiri. HABARI MPYA DAILY:https://bit.ly/3c3bEDc HABARI ZA MICHEZO: https://bit.ly/2TAgnWx HABARIZA WASANII: https://bit.ly/2X2f84R HABARI ZA SIASA: https://bit.ly/36r0xCW Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/Kidanistars Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars