Gooooal Raizin Hafidh dk ya 01 Coastal Union Gooooool Kagere dk ya 49 Simba Goooooool Kagere dk ya 67 Simba MCHEZO wa ligi kuu kati ya #CoastalUnion ya Tanga na Simba unaochezwa uwanja wa Mkwakwani kwa sasa umekamilika. Coastal Union wametangulia kupachika bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Raizin Hafidh dk ya kwanza baada ya beki wa Simba Erasto Nyoni kujichanganya na mlinda mlango Manula. Kipindi cha pili dakika ya 49 Meddie Kagere anasawazisha bao kwa mkwaju wa penalti. Kagere anaandika bao la pili wa Simba dakika ya 67 akimalizia pasi ya Clatous Chama Hili linakuwa ni bao la sita kwa mlinda mlango Aish Manula kutunguliwa ndani ya ligi kuu #CoastalUnion #Simba #LigiKuuTanzaniaBara #MK14