Content removal request!


Refa Akataa Bao La Kagere Taifa Simba 0-0 Lipuli FC

Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars SIMBA SC imelazimishwa sare ya bila kufungana na Lipuli FC ya Iringa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Kwa sare hiyo, mabingwa hao watetezi wanajiongezea pointi moja na kufikisha 27 baada ya kucheza mechi 12, wakiendelea kushika nafasi ya tatu nyuma ya watani wao wa jadi, Yanga SC wenye pointi 29 za mechi 11 na vinara, Azam FC wenye pointi 33 za mechi 13. Kwa Lipuli FC inayofundishwa na Nahodha wa zamani wa Simba SC, Suleiman Abdallah Matola sare ya leo inawafanya wafikishe pointi 13 katika mechi ya 14, wakiwa bado katika eneo la hatari la kushuka daraja, nafasi ya 14 kwenye Ligi Kuu ya timu 20. Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni, Paul Bukaba/James Kotei dk39, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Shiza Kichuya/Haruna Niyonzima fk75, Cloutus Chama, Meddie kagere, John Bocco na Hassan Dilunga/Rashid Juma dk46. Lipuli FC; Mohamed Yussuph, William Lucian ‘Gallas’, Paul Ngelema, Ibrahim Job/Novaty Lufunga dk62, Ally Sonso, Freddy Tangalu, Steven Mganga, Mussa Nampaka/Shaaban Ada dk66, Paul Nonga, Zawadi Mauya na Miraji Athumani.