Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara akizungumzia kuhusu hali ya golikipa namba moja wa klabu hiyo Aishi Manula, aliyeumia jana kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania na kutolewa nje ya uwanja. "Baada ya mchezo kuisha daktari ameniambia kuwa kila kitu kipo sawa, amepelekwa hospitali kufanyiwa vipimo na tunasubiri majibu. Manula ni mchezaji muhimu sana na nina uhakika ataweza kucheza Sudan." Kocha mkuu wa klabu ya Simba Didier Gomes akizungumzia kuhusu golikipa Aishi Manula.