Content removal request!


VIDEO: HAIJAWAHI TOKEA MWANZO MWISHO MAPOKEZI YA SIMBA SONGEA YAVUNJA REKODI|CEO WA SIMBA ASHANGAZWA

MASHABIKI wa Simba leo wamejitokeza kwa wingi kuipokea timu hiyo ambayo imewasili leo Juni 23, Songea. Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Azam FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho.  Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majimaji, Juni 26. Ni Simba ambao ni mabingwa watetezi wa taji hilo walitwaa msimu uliopita baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC ilikuwa Uwanja wa Nelson Mandela. Gomes amesema:"Tunatambua kwamba Azam FC ni timu bora kwani ina wachezaji wazuri hivyo wachezaji wangu nimewaambia kwamba wanapaswa kufanya kazi kwa umakini kusaka ushindi," .