Content removal request!


USAJILI: YANGA Yamsajili MSHAMBULIAJI wa MBAO FC, WAZIRI JUNIOR

MSHAMBULIAJI namba moja wa Klabu ya Mbao FC, Waziri Junior leo Agosti 2, ametambulishwa rasmi kuwa mali ya Yanga. Junior amesaini dili la miaka miwili akiwa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake wa mwaka mmoja kukamilika ndani ya Mbao FC. Ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2019/20 alijenga ushkaji na nyavu akifunga jumla ya mabao 12 akiwa ni namba moja ndani ya kikosi hicho. Mchezo wa mwisho kuvaa jezi ya Mbao FC ilikuwa jana, Agosti Mosi, mbele ya Ihefu kwenye mchezo wa playoff uliochezwa Uwanja wa Kirumba ambapo alifunga mabao mawili. Timu yake ya Mbao aliyokuwa anaitumikia awali akiwa ni nahodha imeshushwa jumla itashiriki Ligi Daraja la Kwanza kwa faida ya mabao ya ugenini ambayo Ihefu wameipata. Mchezo wa kwanza Ihefu ilishinda mabao 2-0 Mbeya na jana ilifungwa mabao 4-2 na kushinda kwa faida ya mabao ya ugenini. Huu unakuwa ni usajili wa nne kwa Yanga msimu huu ilianza na Zawad Mauya kutoka Kagera Sugar ikafuata kwa Bakari Mwamnyeto kutoka Coastal Union na Yassini Mustapha wa Polisi Tanzania. Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars HABARI MPYA DAILY:https://bit.ly/3c3bEDc HABARI ZA MICHEZO: https://bit.ly/2TAgnWx HABARIZA WASANII: https://bit.ly/2X2f84R HABARI ZA SIASA: https://bit.ly/36r0xCW Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/Kidanistars Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars