Content removal request!


SimbaSC ikimchaKAZA Asec Mimosa 3-1,Tazama magoli yote,Sakho,Banda,Kapombe,Simba vs Asec, Simba leo

Sakho Nascimento Pele. Goli la Pele lilifungua kinywa pale kwa mkapa liliashiria leo itakuwa siku njema na kesho Valentine itakuwa ni kumwaga na kuchota upendo kwasababu hakika jua linazama likiwa na tabasamu maridhawa,likiwa linaushahidi kwamba rangi Nyekundu ni ya kipekee. Pia goli hili la Pele limeacha uchungu,limeacha huzuni kwasababu Kuna upande ulikuwa unaomba Mwana wa Kondoo kunyongwa,Mwana wa Kondoo kupewa chakula kibaya na zaidi kufukuzwa zizini. Wakati Jua linaenda kuzama dunia nzima inafahamu kuna Pele mmoja yule wa Brazil yule ambaye ni mfalme wa soka lakini pale Kijiji kwetu msimbazi tunamjua Pele mmoja ambaye Mara nyingi tunamuita kwa heshima yote yaani Sakho Nascimento Pele kwasababu goli lake la bicycle kick limeleta furaha kwa yule shabiki aliyevaa jezi nyekundu,limeleta huzuni kwa yule shabiki aliyevaa jezi ya Njano.