Content removal request!


Kocha Simba, Tumeshinda 5-0, Kagere, Chama, Okwi na Bocco

Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars MSHAMBULIAJI Mganda, Emmanuel Okwi ameanza kuonyesha cheche katika msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kufunga mabao matatu katika katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani usiku wa leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Kwa ushindi huo ulionakshiwa na mabao mengine mawili ya Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere na mzawa, Adam Salamba, Simba SC inafikisha pointi 23 baada ya kucheza mechi 10, ikiendelea kuwa nyuma ya Azam FC inayoongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 27 za mechi 11. Okwi aliifungia Simba SC bao la kwanza dakika ya saba akimalizia krosi ya beki wa kulia, Shomari Kapombe baada ya kazi nzuri iliyofanywa na kiungo Shiza Ramadhani Kichuya. Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars #RuvuShooting #Simbasc