Content removal request!


Yanga 2-1 Lipuli, ONA YANGA Walivyoshuka Taifa vs Lipuli FC Ligi Kuu

Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars YANGA SC imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya timu ngumu kwao kihistoria, Lipuli FC ya Iringa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kwa ushindi huo, Yanga SC nayofundishwa na Mbelgiji Luc Aymael anayesaidiwa na mzawa, Charles Boniface Mkwasa, kocha wa Fiziki, Riedoh Berdien kutoka Afrika Kusini na kipa wa zamani wa klabu, Manyika Peter anayewanoa walinda milango wa timu hiyo – inafikisha pointi 34 baada ya kucheza mechi 17 na kupanda nafasi ya tatu. Sasa inazidiwa pointi nne na Azam FC na pointi 16 na vinara na mabingwa watetezi, Simba SC ambao hata hivyo kwa pamoja wamecheza mechi mbili mbili zaidi. Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Metacha Mnata, Juma Abdul, Jaffar Mohamed, Lamine Moro, Said Juma ‘Makapu’, Papy Kabamba Tshishimbi, Ditram Nchimbi/Deus Kaseke dk71, Haruna Niyonzima/Ally Mtoni dk81, Yikpe Gislain/David Moringa ‘Falcao’ dk61, Balama Mapinduzi na Bernard Morrison. Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Lipuli FC; Deogratius Munishi ‘Dida’, David Kameta, Paul Ngalema, Peter Mwangosi, David Mwasa, Novaty Lufunga, Said Mussa/Zubery Ada dk72, Freddy Tangalu, Paul Nonga, Daruweshi Saliboko na Keneth Masumbuko. Twitter: https://twitter.com/Kidanistars Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars