Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars SIMBA SC imeanza mapema utawala katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Septemba 26, 2019. Kikosi cha Kagera Sugar kilikuwa; Said Kipao, Mwaita Gereza, David Luhende, Hassan Isihaka, Erick Kyaruzi/Juma Nyoso dk46, Zawadi Mauya, Awesu Awesu, Ally Ramadhani, Evarigestus Mjwahuki, Abdallah Seseme na Yussuf Mhilu/Peter Mwalyanzi dk50. Simba SC; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Tairone Santos, Serge Wawa, Gerson Fraga ‘Viera’, Deo Kanda/Miraj Athuman dk62, Muzamil Yassin, Meddie Kagere/Wilker Da Silva dk87, Sharaf Eldin Shiboub na Ibrahim Ajibu/Hassan Dilunga dk71. Mechi nyingine ya Ligi Kuu, Lipuli FC wamelazimishwa sare ya 2-2 na Mbeya City Uwanja wa Samora mjini Iringa. Mabao ya Lipuli FC yamefungwa Issa Rashid dakika ya 15 na Paul Nonga dakika ya 77, wakati ya Mbeya City yamefungwa na George Chota dakika ya 47 na Ibrahim Mwakamole dakika ya 86. Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/Kidanistars