Nimepata taarifa za El Merreikh kujumusha wachezaji 3 kwenye mechi vs Simba ingawa walifungiwa miezi 6 baada kusaini kandarasi na vilabu 2 tofauti (El Hilal na El Merreikh) wachezaji hao ni Mohamed AlRashed Mahamoud, Ramadan Agab, Baljit Khamis Mohamed Kwa mujibu wa kanuni ya CAF ya VI(10) timu itakayochezesha mchezaji asiye halali itapoteza mchezo na kuondolewa mashindanoni 👉 Kwa mujibu wa barua ambayo El Merreikh waliyopewa ni wazi kuwa walichezesha wachezaji ambao hawakustahili Hivyo Simba wana haki ya kwenda kushtaki CAF SIMBA huenda ikapata ushindi wa mezani dhidi ya Al Merrikh kutokana na timu hiyo ya Sudan kudaiwa kuwatumia wachezaji wawili ambao hawakupaswa kucheza katika mchezo baina yao uliochezwa jijini Khartoum, Jumamosi iliopita ambao uliisha kwa sare tasa. Taarifa za uhakika ambazo uongozi wa Simba umedai kuzinasa kutoka Sudan kwa ushahidi wa nyaraka mbalimbali, zimeonyesha kuwa wachezaji hao Ramadan Agab na mwingine ambaye jina lake wanalisaka, walicheza mechi hiyo huku wakiwa wanatumikia adhabu ya kufungiwa miezi sita waliyopewa na Chama cha Soka Sudan (SFA) Ushahidi wa barua ambao Simba wameupata na kuionyesha Mwanaspoti nakala, unaonyesha kuwa SFA iliwafungia wachezaji hao kwa muda wa miezi sita kwa kosa la kusaini mikataba katika timu mbili tofauti, adhabu ambayo inaishia katikati ya Aprili "Hii ni nakala ya uamuzi. Kimsingi wachezaji hao wawili walisaini mikataba miwili tofauti na Al Merrikh na Al Hilal na wamefungiwa kucheza kwa muda wa miezi sita. Barua hii ni ya Katibu Mkuu wa Al Merrikh ambayo walimpa kocha kwamba anaweza kuwatumia wachezaji wawili waliofungiwa. Wachezaji hao hawakucheza mechi yoyote ya Al Merrikh hadi sasa. Wamefungiwa kucheza hadi katikati ya Aprili. Wamefanya uamuzi wao wenyewe," alisema mtendaji mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez. Ikiwa itabainika ni kweli Al Merrikh waliwachezesha wachezaji ambao hawakustahili kucheza, itaondolewa mashindanoni "Timu itakayomchezesha mchezaji aliyesimamishwa au asiyeruhusiwa itahesabika imepoteza mchezo husika na moja kwa moja itaondolewa mashindanoni ikiwa kamati ya mashindano ya Caf itajiridhisha na hoja zitakazowasilishwa," inasema kanuni ya saba.