Azam FC wamekula kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Namungo FC, katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa kwenye Dimba la Azam Complex, Chamazi. Magoli ya Namungo yametoka kwa Pius Buswita dakika ya 10, Hashim Manyanya dakiak ya 19 na Reliants Lusajo dakika ya 50 huku goli la kufutia machozi likifungwa na Ayoub Lyanga dakika ya 70.