Content removal request!


Ninja asimulia jinsi alivyopigwa Congo na walinzi kisa picha ya Hersi

Baada ya beki wa kati, Abdallah Shaibu 'Ninja' kumalizana na Lubumbashi Sport ya DR Congo, ametaja mipango aliyonayo kwa msimu ujao, huku akisimulia kisa kupiga picha na Injinia Hersi Said. Ninja alijiunga na Lubumbashi Sports kwa mkataba wa miaka miwili, akitokea Yanga ameutumikia mmoja, kisha ameomba kuondoka akitoa sababu ni usalama mdogo wa maisha ya DR Congo. "Japo kuna timu tatu za DR Congo zinahitaji huduma yangu, labda nipewe pesa ndefu, hata nikikaa kwa shida familia yangu Tanzania iwe salama, nje na hapo zipo timu hapa nyumbani zinahitaji huduma yangu nitazipa nafasi, kwanza Ligi Kuu Bara ni maarufu na inafuatiliwa na nchi mbalimbali," amesema na kuongeza; "Wakati nafika mara ya kwanza, niliambiwa kutembea mwisho saa 3:00 usiku, kila mtaa unapita unakutana na askari, sasa kuna wakati mwingine unaweza ukatoka kutafuta chakula cha Kitanzania, saa 3:00 ikikukutia nje ya nyumba yako ni shida." Hata hivyo, Ninja amesema hatosahau kipigo alichopigwa na walinzi wakati akiingia uwanjani kwenda kukutana na Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said. #samiasuluhuhassan #simbasc #yangasc #mashabiki #nbcpremeireleague #cafchampionsleague #cafconfiderationcup #ikulumawasiliano #entertainment #music #news #yangasc #simbasc #cafchampionsleague #mayele #highlights #cafconfiderationcup #riversunited #mashabiki #yangaleo #yanga #timuyawananchi #daimambelenyumamwiko #entertainment #music #news #magoliyasimba #magoliyayanga #magoliyote #magoliyamayele #mayele #aziziki #manara #manaraleo #ikulumawasiliano #magufuli #kikwete #mayele #singidabigstars #magoliyamayele #magoliyasimba #magoliyayanga #highlights #azamsportsfederationcup #chama #Shot #mamelodisundowns #alahlytv #alahlysc #miraj