Content removal request!


Taifa Stars Kuikabili Cape Varde kwa Dreamliner!!

#TAIFASTARS Taifa Stars Kuikabili Cape Varde kwa Dreamliner!! Serikali imekubali kutoa ndege yake aina Boing 787 Dreamliner kwa ajili ya kuisafirisha timu ya taifa ya Tanzania –Taifa Stars kwenda Mjini Praia Cape Varde kwa ajili ya mchezo wa raundi ya tatu ya michuano ya kufuzu kwa ajili ya michuano ya AFCON ya Cameroon mapema mwakani. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe amewaambia waandishi wa Habari kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya kufanya tathmini ya mazingira ya michezo miwili baina ya stars na Cape Varde na mazingira ya ndege za kawaida za biashara. Kwa upande wake Rais wa TFF Wallace Karia ametoa wito kwa wadau wa soka nchini kujitokeza kwa wingi kusafiri na timu hiyo kutokana na uwepo wa usafiri wa moja kwa moja kwenda Mjini Praia, nchini Cape Varde. Taifa Stars itashuka Dimbani October 12, mwaka huu kuumana na Cape Varde katika mchezo wa Raundi ya tatu ya kundi L ambalo pia linaundwa na timu za Uganda na Lesotho. bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://ww.youtube.com/c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Suazi1 http://www.youtube.com/c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari INSTAGRAM: https://www.instagram.com/globalpubli.