Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars KIKOSI cha Simba Desemba Mosi kimereja salama ndani ya ardhi ya Tanzania baada ya kuanza safari jana Novemba 30 kutoka mji wa Jos Nigeria na leo kilianzia safari Abuja kabla ya kuibukia Kilimanjaro. Wawakilishi hao wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika walishinda bao 1-0 dhidi ya Plateau United kwenye mchezo wa awali. Mchezo huo ulichezwa Novemba 29 ulikuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90 huku ukitawaliwa na matukio mengi ya nje ya uwanja ikiwa ni pamoja na kuzuia tukio hilo kurushwa mubashara kupitia Television. Baada ya ushindi wa mchezo wa kwanza, Simba wanatarajiwa kurudiana Desemba 5, Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa pili ikiwa itashinda itasonga mbele kwenye hatua ya mtoano. Mratibu wa Simba, Abbas Ally amesema kuwa wachezaji wote wapo salama jambo linalowapa nguvu kupambana kuelekea mchezo wao wa pili ambao utakuwa na ushindani mkubwa. HABARI MPYA DAILY:https://bit.ly/3c3bEDc HABARI ZA MICHEZO: https://bit.ly/2TAgnWx HABARIZA WASANII: https://bit.ly/2X2f84R HABARI ZA SIASA: https://bit.ly/36r0xCW Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/Kidanistars Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars