Yanga SC leo wametangazwa kuwa Mabingwa wapya wa Ligi Kuu baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo uliyochezwa Benjamin Mkapa, Yanga ambao waliukosa Ubingwa kwa miaka minne mfululizo wametwaa Ubingwa wao wa 28 leo wakiwa na michezo mitatu mkononi, Yanga leo wamefikisha jumla ya point 67 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ile hata kama watapoteza michezo yao mitatu iliyosalia, Simba anawafuatia akiwa na point 51 kacheza michezo 25 hata akishinda michezo yote mitano atakuwa na point 66.