Content removal request!


Simba Waifunga 3-0 Ruvu Shooting, Cheki Walivyotua Uwanjani

Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars MABINGWA watetezi, Simba SC leo NOV 23, 2019 wameiadhibu Ruvu Shooting baada ya kuichapa mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam. Nyota wa mchezo wa leo alikuwa ni mshambuliaji Miraji Athumani ‘Madenge’ aliyefunga mabao mawili, huku linguine likifungwa na beki Mbrazil, Tairone Santos da Silva. Na kwa ushindi huo, Wekundu wa Msimbazi wanafikisha pointi 25 katika mchezo wa 10 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu ikifuatiwa na Kagera Sugar yenye pointi 23 za mechi 11, wakati Ruvu Shooting inabaki pointi zake 15 baada ya kucheza mechi 12. Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/Kidanistars Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars