Content removal request!


TAMKO LA TFF KUHUSU SIMBA SC na YANGA, WALIOLIPA VIINGILIO, TPLB YAPEWA MAELEKEZO

Shirikisho ka Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesikitishwa na kilichotokea na kusababisha mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba SC na Yanga SC iliyokuwa ifanyike jana iahirishwe. TFF inapenda kuomba radhi kwa wadau wote, waliolipa viingilio kuingia uwanjani, waliokuwa wakisubiria kuangalia kwenye televisheni, kusikiliza redioni na watoa huduma mbalimbali. Kwa hali hiyo TFF imetoa maelekezo kwa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kutoa taarifa kwa kina kuhusu kuahirishwa kwa mchezo huo, pamoja na kushughulikia hatma ya wapenzi wa mpira wa miguu waliolipa viingilio kuingia uwanjani. Tunawaomba wapenzi wa mpira wa miguu kuwa watulivu wakati jambo hili linashughulikiwa kwa haraka kwa taratibu za kikanuni, lakini huku tukishirikiana kwa karibu na wadau wote ikiwemo Serikali. TFF imekuwa ikishirikiana na Serikali kama mdau wake mkuu, na itanedelea kushirikiana nayo kuhakikisha kwamba mechi zote za mpira wa miguu zinafanyika kwa amani na usalama. Pamoja na jambo hili kuendelea kushughulikiwa kikanuni kama tulivyoilekeza Bodi ya Ligi, TFF inaendelea kufanya vikao mbalimbali na vyombo vya Serikali kuhusu tukio hilo, pia itakutana haraka na klabu hizo (Simba na Yanga).