Content removal request!


KAGERA SUGAR YALALA NA VIATU, YAPIGWA 2-0 NA RUVU SHOOTING

KAGERA SUGAR YALALA NA VIATU, YAPIGWA 2-0 NA RUVU SHOOTING Na Omary Mngindo, Mlandizi Pwani Tanzania- Feb 8 TIMU ya soka ya Ruvu Shooting ya Mlandizi Kibaha Pwani Tanzania Alhamisi ya Feb 8 imeendelea kuutumia vema uwanja wake wa nyumbani baada ya kuilaza na "VIATU" Kagera Sugar ya mkoani Kagera kwa mabao 2-0. Mchezo huo uliokuwa mkali na kuvutia kwa muda wote, washindi walioutumia uwanja wa nyumbani, ilibidi wasubiri mpaka kipindi cha pili kujipatia mabao hayo yaliyofungwa na Mcha Khamis kwa njia ya penati, wakati bao la pili likiwekwa kambani na Alinanuswe Martin akimalizia krosi kutoka magharibi ya uwanja. Mpaka dakika 90 za mwamuzi wa mchezo huo, Shooting imejipatia ushindi wa pili mfululizo katika uwanja wake wa nyumbani baada ya kuibuka na idadi kama hiyo dhidi ya Mbao FC ya jijini Mwanza uliochezwa majuma hivi karibuni. MWISHO.R