MAKOSA MATATU GOLI LA PRISONS DHIDI YA SIMBA . Kwanza kabisa aliyerushiwa mpira hakuwa amekabwa kabisa.. Wachezaji wote wa Simba hawakuwa eneo la mpira, walikimbilia nyuma. . Pili, Joash Onyango ameshindwa kumkaba vizuri Mbangula.. Kabla ya Krosi kupigwa, Mbagula alikuwa nyuma ya Onyango.. Ila baada ya mpira kukaribia alisogea na kupiga kichwa mbele ya Onyango.. . Tatu, Aishi Manula alisogea kwenda wapi? Kuondoka kwenye eneo lake bila kuwa na hesabu sahihi za kwenda kuudaka mpira ilikuwa kosa.. Ila kosa kubwa zaidi ilikuwa kusita na kurudi.. Hii ni ishara kwamba hakuwa na uhakika na anachokifanya.. Ameshindwa kusahihisha makosa ya mabeki wake... . Mwisho tumpongeze Mbangula kwa bonge ya header.. Aliruka kwa ufasaha.. Akapiga kichwa chenye nguvu.. Akachagua angle sahihi.. Bonge ya goli.. . . NB: NATAMANI KUONA TIMU NYINGINE YA VPL IKICHEZA NA PRISONS BILA NYOTA WAKE SABA.. TUONE ITAKUWAJE..