Content removal request!


MO DEWJI ATANGAZA KUJIUZULU SIMBA SC

Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars SIMANZI na hali ya sintofahamu imeanza kuingia pale Msimbazi. Ndio, Simba imepoteza taji la kwanza msimu huu baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar, katika fainali ya Kombe la Mapinduzi. Mchezo huo umepigwa jana usiku kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, ambapo Simba ikiwa na mastaa wake tegemeo ilionekana kuzidiwa kila idara na Mtibwa Sugar, ambao waliingia fainali baada ya kuichapa Yanga kwa mikwaju ya penati huku Simba nayo ikiwaondoa mabingwa watetezi, Azam FC. Hata hivyo, wakati mashabiki na wapenzi wa Simba wakiugulia maumivu kwa kipigo hicho, mambo yamezidi kuharibika zaidi baada ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, Mohammed Dewji (Mo) kutangaza kuachia ngazi kutokana na kutoridhishwa na matokeo hayo. Katika taarifa yake kupitia ukurasa wake wa Twitter muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mo alisema: “Baada ya kulipa mishahara inayofikia Sh4 bilioni kwa mwaka, najiuzulu wadhifa wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi. Nitabaki kuwa mwekezaji na nitazingatia kukuza miundombinu ya soka la vijana.” Mtibwa ambao walionekana kucheza soka safi na kumiliki mchezo huo, ilipata bao lake la ushindi dakika ya 38 kupitia kwa Awadh Salum, ambaye alipenya katikati ya msitu wa walinzi wa Simba. Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/Kidanistars Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars