Lakini haukuwa ushindi mwepesi, kwani Azam FC ililazimika kusubiri hadi dakika 30 za nyongeza kupata tiketi ya kwenda fainali, baada ya kubanwa kwa sare ya 0-0 ndani ya dakika 90. Mabao ya Azam FC ambayo leo ilimkosa kinara wake wa mabao, Shaaban Iddi Chilunda yamefungwa na Ditram Nchimbi dakika ya 92 na beki Mzimbabwe, Bruce Kangwa dakika ya 100.