Content removal request!


MAMBO 10 YA KITAALAMU ALIO YAONA ALI KAMWE SIMBA IKIPIGA DODOMA 3 -1|CHAMA ANA ASSIT 13

Mambo 10 nilioyaona Simba vs Dodoma 1: WHAT A MATCH. Tactically, Technically makocha na wachezaji wametupa dakika 90 zilizoshiba. Mechi ya nguvu, kasi na maarifa ya kutosha..  2: Kocha wa Dodoma Jiji, Mbwana Makata aliingia na 4-2-4 akiwa na viungo wawili tu katikati ya kiwanja. Watu wanne wa juu wakiwa bora sana kwenye pressing 🙌 Game Plan ilikuwa sahihi, 'Quality' ikatofautisha ubao wa matokeo. Nafasi ambazo Dodoma walizichezea, Simba walizitumia. 3: Dakika 45 za kwanza, Didier Gomes alibaki na sytem ya 4-2-3- 1 lakini akabadili style of Play kidogo. Chama akaenda pembeni, Bwalya akacheza zone ya 14. Timu ikaonekana nzito kidogo 'kulink' kutoka kati kuingia phase ya 3 ya kiwanja. Nini alifanya? 4: Akamtoa Muzamir Yassin akamuingiza Morrison. Chama akarudi kwenye zone ya 14, Bwalya akarudi kati. Timu ikalainika, nafasi zinakapatina. 5: Again, Simba wamethibitisha tena nilichowahi kukisema. Ni timu hatari pindi inaposhambuliwa. Mpinzani akitawanyika wana watu wazuri wa kutega kwenye maeneo ya wazi. Wakiupata mpira.. hawachezi, wanashambulia.  6: CHAMA 🐐.. Damu ya Zambia. mwili wa Hispania. Akili ya Brazil.. Alichobakisha ni kutoa asali na maziwa kwenye miguu yake..  What A Player 🙌 Anaufanya mchezo wa mpira uonekana mrahisi sana. Yuko Sharp kwenye kujitengenezea nafasi na ni mtulivu kwenye maamuzi yake  7:  Ule mguu wa kushoto wa Larry Bwalya una 'vision' ya ajabu sana🙌 Ana utulivu sana. Anaimeza presha ya Opponent kwa ustadi wa aina yake. Ile pivot yake na Nyoni inawapa uhakika Simba wa kumiliki mpira kwa muda mwingi wa mchezo 8: Justine Omary🙌 Yule beki wa kati wa Dodoma Jiji.. Ni mpambanaji sana. Ana kimo kizuri, ana nguvu na timing yake ni nzuri sana. Akisukuma kidogo kwenye kutafuta kasi, he is one of the best tunaoweza kuwategemea kwa baadae 9: Miquissone 👍 Katika ubora wake wa kila siku. Dodoma walimpa mechi ngumu akawafunga bao gumu. Ule ndio ubora unaowabeba Simba wanapokuwa katika nyakati ngumu kiwanjani 10: Mkandala 👍 Alipambana sana kumvuruga Muzamir katikati ya kiwanja. Wale mabeki wa pembeni wa Dodoma, George Wawa na Ngalema wamevuja sana jasho. Well done kwao.. Nb: Tar 8 bebeni Tende tu.. Ftari mtaipata KWA MKAPA 😀