Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars KLABU ya Namungo imejikuta ikikata tiketi ya kutinga hatua ya pili ya mtoano ya Kombe la Shirikisho Afrika wakiwa hotelini baada ya mchezo wao wa marudiano kufutwa dhidi ya Al Rabita. Taarifa kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ni kwamba Shirikisho la Soka Afrika (Caf) imetangaza kuufuta mchezo huo wa marudiano ambao wenyeji walitakiwa kuwa Rabita sababu kubwa ikiwa kushindwa kwa kugharamiwa kwa waamuzi wa mchezo huo ambao ulitakiwa kupigwa baadaye jioni katika Uwanja wa Chamazi Complex nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Rabita waliomba mchezo huo upigwe katika uwanmja huo baada ya kushindwa kuchezwa nchini kwao Sudan kutokana na sababu za kiusalama ambapo Shirikisho la Soka Afrika (Caf) waliridhia ombi hilo. Taarifa ya TFF imesema Caf imetangaza uamuzi huo baada ya Chama cha Soka Sudan Kusini (SSFA) kushindwa kukamilisha taratibu kuhusu waamuzi waliopangwa kuchezesha mechi hiyo. "CAF wamefuta mechi ya kombe la Shirikisho kati ya Al Rabita FC Juba na Namungo FC iliyokuwa ichezwe leo jijini Dar es Salaam."imesema sehemu ya taarifa hiyo ya TFF HABARI MPYA DAILY:https://bit.ly/3c3bEDc HABARI ZA MICHEZO: https://bit.ly/2TAgnWx HABARIZA WASANII: https://bit.ly/2X2f84R HABARI ZA SIASA: https://bit.ly/36r0xCW Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/Kidanistars Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars