Dakika 90 za mchezo wa Ligi Kuu Bara baina ya Yanga na Stand United umemalizikwa kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa bao 4-3. Mechi hiyo iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam imeshuhudiwa mabao ya Yanga yakikwekwa kimiani na Mrisho Khalfan Ngassa, Andrew Vincent na Deus Kaseke. Wakati huo mabao matatu ya Stand United 'Hat Trick' yamewekwa kimiani na Alex Kitenge ambaye ameondoka na mpira. Ushindi huo kwa Yanga unawafanya kufikisha jumla ya alama 6 sawa na Stand United United iliyopoteza. Wakati huo huo Mbeya City iliyokuwa Uwanja wake wa nyumbani ikicheza na Alliance School ya Mwanza imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0. Mbeya City wamejipatia mabao hayo kupitia kwa Victor Hanganya na Eliud Ambokile.