Sare zimeendelea kutawala katika mechi za Ligi Kuu Bara inayowakutanisha Yanga na Namungo baada ya leo pia timu hizo kutoka sare ya bao 1-1. Mabao ya Obrey Chirwa na Saido Ntibazonkiza yamefanya timu hizo kufikisha mechi tano za Ligi Kuu Bara tangu 2019 bila yoyote kuwa mbabe wa mwenzake. Chirwa aliipatia Namungo bao dakika ya 52 kwa shuti Kali lililomshinda kipa wa Yanga, Diarra. Dakika ya 59 Yanga ilifanya mabadiliko ya wachezaji watatu kwa mpigo baada ya kuwatoa Mukoko Tonombe, Jesus Moloko na Farid Mussa na kuwaingiza Said Ntibazonkiza 'Saido', Deus Kaseke na Yusuph Athuman lakini dakika tano baadae wakamtoa Kibwana Shomari na kumuingiza David Brayson wakati kwa upande wa Namungo alitoka Shiza Kichuya na nafasi yake kuchukuliwa na Hashim Manyanya.