SIMBA inafanya mambo yake kimya kimya na juzi ikaonyesha ubabe kwa watani wao wa jadi, Yanga baada ya kufanikiwa kuidaka saini ya beki wa kati, Ibrahim Ame aliyekuwa anaichezea Coastal Union msimu uliopita. Ame, ambaye alikuwa pacha wa Bakari Mwamnyeto na kuwatuliza mastraika tishio, amesaini mkataba wa miaka miwili juzi Jumanne. Usajili huo sio kikumbo tu kwa Yanga bali hata Polisi Tanzania na Coastal Union ambao, inaelezwa kwamba wao ndio walikuwa wametuma tiketi ya boti kwa mchezaji huyo kutoka Zanzibar. Picha lenyewe lilikuwa hivi: Unaambiwa vurumai iliyotokea Bandarini, Dar es Salaam haikuwa ya kawaida kwani makomando wa timu zote tatu walitinga eneo hilo na kila upande ukimsubiri beki huyo ili kwenda kumalizana naye na kumsainisha. Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars HABARI MPYA DAILY:https://bit.ly/3c3bEDc HABARI ZA MICHEZO: https://bit.ly/2TAgnWx HABARIZA WASANII: https://bit.ly/2X2f84R HABARI ZA SIASA: https://bit.ly/36r0xCW Instagram: https://www.instagram.com/kidanistars Facebook: https://www.instagram.com/kidanistars Twitter: https://twitter.com/Kidanistars Subscribes:https://www.youtube.com/c/KidaniStars