MASHABIKI RUVU SHOOTING WAKISHANGILIA USHINDI WA KWANZA DHIDI YA NDANDA FC Na Omary Mngindo, Mlandizi, Kibaha Vijijini, Pwani, Tanzania- Nov 18 BAO la pekee la timu ya soka ya Ruvu Shooting dhidi ya Ndanda Fc ya Mtwara lililofungwa na Abdulhaman Mussa kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) limepokelewa kwa shangwe, furaha na vifijo kutoka kwa mamia ya mashabiki wa timu hiyo wengi wao wakiwa vijana waliojiunga na Kikosi cha JKT kwa ajli ya mafunzo. Bao hilo lililofungwa kwa mkwaju wa penati na nyota huyo aliyekuwa mfungaji bora katika Ligi ya msimu uliopita akifungana na kiungo aliyekuwa anakitumikia kikosi cha Yanga Simon Msuva, limeiwezesha timu hiyo kupata ushindi wa kwanza kwenye kinyang'anyiro hicho tangu kuanza kwa ligi ya msimu huu. MWISHO.