Content removal request!


#BREAKING: MORRISON Afungiwa MECHI TATU, Apigwa FAINI, Kuikosa SIMBA vs YANGA...

#BREAKING: MORRISON Afungiwa MECHI TATU, Apigwa FAINI, Kuikosa SIMBA vs YANGA... Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara imemfungia mchezaji wa Simba, Bernard Morrison, kutocheza Mechi tatu na kutozwa faini ya shilling laki tano baada ya kukaa kikao oktoba 27, mwaka huu na kupitia michezo mbalimbali ikiwemo mchezo wa Simba dhidi ya Ruvu Shooting uliochezwa oktoba 25 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Morrison amefungiwa baada ya kukutwa na kosa la kumpiga ngumi mchezaji wa Ruvu Shooting Juma Nyosso katika mchezo huo uliochezwa oktoba 25 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Tukio hilo lilitokea baada ya mpira kusimama dakika ya 72, kutokana na wachezaji wa timu zote mbili kuwa kwenye mzozo uliotokana na mwamuzi kuamua Simba ipige penalti baada ya mchezaji Luis Miquissone kuonekana akichezewa faulo ndani ya 18. Morrison mwenye pasi moja ya bao kati ya 14 yaliyofungwa na Simba kwa msimu wa 2020/21, alionekana akimpiga ngumi mchezaji wa Ruvu Shooting, Juma Nyosso kwenye mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Uhuru wakati timu yake ikichapwa bao 1-0. ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx ⚫️ VISIT AMAZON: https://www.amazon.com/shop/globaltvonline ⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI? ⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE ( +255 784 888982), ( +255 713 837506) ⚫️ Email: globaltvbest@gmail.com OR abbymrisho@gmail.com ⚫️ OUR PLAYLISTS: ⚫️ HABARI MPYA DAILY:shorturl.at/mnux2 ⚫️ HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA: http://bit.ly/mikasa_ya_kusisimua ⚫️ GLOBAL RADIO TV: http://bit.ly/255globalradio ⚫️ EXCLUSIVE INTERVIEW: http://bit.ly/exclusive_interviews ⚫️ Subscribe Global TV http://bit.ly/globaltvonline